Mambo ya Sheria ya Uchaguzi....Politricks


Dk. Slaa alipua bomu
Adai mchezo mchafu umefanyika sheria ya uchaguzi
na Irene Mark

KWA mara nyingine, Rais Jakaya Kikwete, amepotoshwa ukweli kuhusu sheria ya gharama za uchaguzi aliyoisaini hivi karibuni katika Ikulu yake jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kuwa baadhi ya vipengele vimeingizwa kinyemela nje ya Bunge, Tanzania Daima Jumatano, imebaini.
Kipengele kilichoingizwa kinyemela bila kujadiliwa na kupitishwa na Bunge mjini Dodoma, ni kile kinachohusu uthibitishwaji wa wajumbe wanaounda timu za kampeni kwa ajili ya wagombea wa urais, ubunge na udiwani.

Wakati Bunge linajadili na kupitisha sheria ya gharama za uchaguzi, sehemu inayohusu uthibitishaji wa timu za wagombea ilijadiliwa na wabunge wote, lakini haikueleza nani anayepaswa kukagua timu za kampeni za wagombea wa nafasi mbalimbali, lakini katika sheria aliyosaini rais, inafafanua watu wanaostahili kukagua timu za kampeni.

Kwa mujibu wa sheria iliyosainiwa kwa mbwembwe na Rais Kikwete, kipengele kinachodaiwa kuchomekwa bila ridhaa ya Bunge, kinaonyesha kuwa timu za kampeni za wagombea urais, zitathibitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, timu za kampeni za wagombea ubunge, zitathibitishwa na Makatibu Tawala wa Wilaya wakati timu za kampeni za wagombea wa udiwani, zitakaguliwa na kuthibitishwa na Makatibu Tarafa

No comments: