HEKA HEKA ZA MILIPUKO YA MABOMU GONGO LAMBOTO

Usiku wa kuamkia leo utabakia kuwa historia kwa wakazi waishio Dar es Salaam haswa wa maeneo ya Gongo la Mboto pamoja na maeneo ya Jirani. Vifo, Majeruhi, Uharibifu wa Mali, Majengo, ndio vilio vikubwa kwa wakazi hawa baada ya kutokea Milipuko Mikubwa ya mabomu katika kambi ya Jeshi huko Gongo la Mboto wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Sala na misaada yetu ya hali na mali ndio ombi la wakazi hawa.
hawa ni baadhi ya Majeruhi walio nusurika katika milipuko ya mabomu huko Gongo Lamboto usiku wa kuamkia leo
baadhi ya wakazi wa maeneo ya gongo la mboto wakitimua mbio ili kuokoa maisha yao

hii ndio hali halisi iliyokuwa huko gongo la mboto, moto utadhani Volcano

Milipuko mikali katika eneo la tukio. wanachi wahaha, wapoteza maisha, uharibifu mkubwa watokea.
Je! Serikali inasemaje kuhusu milipuko hii? Endelea kutembelea blog hii ya jamii..

1 comment:

Anonymous said...

kitu ilifika hadi kimara kaka...tumekimbia kilomita zaidi ya 3 kuokoa maisha yetu..dah!