SAKATA LA UHURU PARK

Halmashauri yaweweseka sakata la Uhuru Park

Na Daniel Mjema,Moshi(GAZETI MWANANCHI)


HALMASHAURI ya Manispaa ya Moshi imesema pamoja na Baraza la Madiwani kupitisha uamuzi wa kumpa mwekezaji hati ya muda ya kumiliki eneo la Uhuru Park mjini Moshi, bado haujathibitishwa rasmi.


Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Dk.Christopher Mtamakaya jana alilazimika kuitisha kikao na waandishi wa habari kujaribu kufafanua uamuzi huo ambao unapigiwa kelele na wanaharakati na wananchi wa Moshi.


“Naomba jamii na vyombo vya habari vielewe kuwa suala la kutoa subtitle (hati usu) ya miaka 33 na kuruhusu mwekezaji huyo kuchukua mkopo wa kuendeleza eneo hilo la wazi limepitishwa na Baraza la Halmashauri,� alisema.


Dk Mtamakaya alisema utekelezaji wa maamuzi ya baraza hilo la madiwani utafanyika baada ya muhtasari wa kikao hicho kuthibitishwa na kuwa na kumbukumbu halali za halmashauri katika kikao kitakachofanyika Juni mwaka huu.


“Mkataba wa awali wa miaka 10 kati ya halmashauri na mwekezaji wa kuendeleza eneo hilo utavunjwa na pande hizo mbili wataingia mkataba mpya ambao utazingatia maamuzi ya kikao hicho cha baraza,� alisema Dk. Mtamakaya.


Kwa habari zaidi bofya hapa

No comments: