JIJI JINO KWA JINO NA WAUZA MADAFU

Baiskeli ya madafu inajali mazingira,ukimaliza kula chupa anabeba mwenyewe kwenda kutupa panapohusika


Muuza Madafu akinitafutia dafu laini,sijui anajuaje kwa nje...


Leo nimehangaika kusaka madafu toka Morocco hadi Msasani kote huko sikupata kitu.Nilipokutana na huyu mheshmiwa muuzaji akanipasulia kuwa wauzaji wamekua adimu mara baada ya kikosi cha mgambo wa jiji kuanzisha kampeni ya kuwakamata kwa madai ya kupiga marufuku biashara zinazochafua jiji...Nilipomuhoji mbona baiskeli za kuuza Ice cream naziona kila kona.......alichukua muda kidogo na kujibu,"ile biashara ya wakubwa sisi walala hoi ndo wanataka watuue kwa umasikini wetu"
Binafsi naona mifuko ya ice cream inachafua jiji zaidi ya madafu ambayo wauzaji wake wanakubali kuhenyeka na maganda yake hadi watakapoenda kutupa mahala husika...
Maisha bora au Bora Maisha kwa kila mTZ???



No comments: