LIFE BILA HAUSGELI INAWEZEKANA???

Nipo katikati ya mjadala na wafanyakazi wenzangu kuhusu sakata la uhaba wa watumishi wa ndani a.k.a beki tatu a.k.a haus geli...Hoja mbali mbali zikaruka,wengine wanasema siku hizi mahaus geli wajeuri,wengine expensive wanataka mkwanja mrefu,wengine hivi wengine vile.....Wakati tunaendelea na mjadala kilongalonga changu kikaita na kupokea napata taarifa kuwa mama Mkwe anaumwa...Kisa??kafanya kazi sana kwa kuwa hausgeli wake ameondoka ghafla na tangu wiki jana anatafuta mwingine bila mafanikio...Juzi kapata mmoja ila alipofikishwa tu nyumbani akaomba simu aweke chip/line yake...eti coinncidentally ile kuweka tu laini akapigiwa simu kuwa kumetokea msiba....

Mabeki tatu viiiiipiiiii???je tunaweza kuishi bila wao???

No comments: