ANA KWA ANA NA DIZAINA 'NGULI' MANJU


Pita pita yangu na misere ya hapa na pale jana imenikutanisha na Nguli wa Mitindo ya Kiafrika nchini Manju Msita.Kwa wadau wa masuala ya ubunifu na wale wanaopenda kutoka maridadi kiAfrika zaidi pasi na kukopi mitindo ya kizungu basi suluhisho ni kuwaona Smart Afrika,Manju designs pale Mikono Art Gallery Chang'ombe(karibu na VETA).
Kama unakumbuka vema mwaka 2004 Manju ndiye alikuwa bingwa wa Taifa wa Mitindo na kutunikiwa tuzo ya heshima....Hebu imagine kuvaa nguo ambayo imedizainiwa na kunakshiwa kwa ajili yako tu....una hakika hutokutana na yeyote mwenye nguo ya namna hiyo kila upitapo watu midomo wazi...!!
Inawezekana,tukiamua!
Its all about Konfidence

1 comment:

Anonymous said...

Huyo Manju mimi namfahamu vilivyo na huwa habahatishi.Kwa kweli inabidi tumuunge mkono maana anachofanya ni ukombozi kwa Mwafrika.Nadhani sasa ni wasaa wa kuuonyesha Ulimwengu kwamba na sisi tunaweza...na hilo nina uhakika Manju analiweza.Ningependa kwa kupitia blog hii nipate namba yake ya simu.