NIPE NIKUPE WIKIENDA

Kaka Fussi Akimkaribisha Mhesmiwa Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila....David ni mwana TYVA
Kaka Mayunga Mkurugenzi wa Breakthrough Business Support alikuwepo kuendesha zoezi la Fundraising kwa ajili ya TYVA...Mayunga aliwahi kuwa mtunza hazina wa TYVA kipindi cha 2004-2006

Mai-waifu wangu akipozi na Michael Dalali wa Agenda Participation(shoto) na Mayunga wa Breakthrough...Dalali aliwahi kuwa Katibu mkuu wa TYVA 2007-2009

Kaka Fredrick Fussi Afisa Miradi wa Ubungo Development Initiative(UDI) akilisakata rhumba na Mwanasheria Chiku katika hafla...wote hawa ni wana TYVA

Asasi ya Tanzania Youth Vision Association(TYVA-Dira ya Vijana) jumamosi iliyopita ilifanya sherehe za kuukaribisha mwaka 2011 katika nustani ya Tamal Hotel iliyopo mwenge jijini Dar es Salaam...Sherehe hizo zilizokwenda kwa staili ya mkia wa jogoo yaani Cocktail zilipamba na shamra shamra za aina yake ikiwemo mahudhurio ya wakongwe wa TYVA wakiwemo viongozi wake wa zamani,waasisi na wanachama wa sasa pamoja na wa zamani.
Katika harambee ya papo kwa papo iliyofanyika Mheshmiwa David Kafulila alijitolea Laptop moja mpya kwa ajili ya shughuli za asasi akisema kwamba anaamini TYVA ilimjenga na anatamani fursa aliyoipata yeye kuwa mwana TYVA waipate vijana wengine.Katika harambee hiyo TYVA pia ilipata modem za intaneti 3,Desktop 2 na kodi ya pang la ofisi.
Wakati naondoka eneo la tukio niliambiwa wahesmiwa Zitto na Mnyika pia wapo njiani kuwasili eneo hilo kujumuika na wana TYVA wenzao. Mnyika aliwahi kuwa katibu Mkuu na Baadae Mwenyekiti wa TYVA kabla ya kuingia rasmi katika siasa mwaka 2004.


No comments: