YALE YALEEE.....

Mitaa ya Kumekucha Sinza kitu kimelia jioni jana...Najiuliza kweli kwa udereva wetu huu hata hizo fly-over zitaweza kutatua tatizo la foleni??Hata ziwe mia Dar nzima bado tutaendelea kugongana kizembe kama inavyoonekana pichani Escudo imelazimisha kukata kona ya kuelekea kanisa la KKKT sinza na mzee mzima mwenye DCM aka gobore akakomaa nae mpaka kikaeleweka ngaaaaaa.....tayari foleni ikawekwa kuanzia Sinza makaburini...


Pichani hiyo gari nayo ikiwa inatanua kukwepa msongamano wa magari yaliyogongana ikajikuta inanikosa kosa mimi ambaye nami kwa ujuaji wangu nilikuwa bize kusaka angle nzuri ya kufotoa....Wadau mnaoshabikia fly-over ndo mjue hivo msije poteza kodi zetu bure...foleni inaletwa na sisi wenyewe na tutaiondoa sisi wenyewe tukiwa makini...


No comments: