ZAIN FAMILY DAY 2010

Jumamosi hii ilikuwa siku ya kujinoma kwa wafanyakazi wa Zain na familia zao pale viwanja vya Leaders.Pichani ni foleni ya mambo ya maakuli..foleni maalum ya watoto yenye vyakula vya dizaini yao...akina chipthi kuku,wali 'maalage' na vikababu na mapochopocho mengine...
Esther Wassira katikati akipozi na mshereheshaji wa shughuli buraza Kibarabara kulia.....

Mdau wa Nipenikupe Yakub Matata a.k.a Kubbu akiratibu kwa karibu masuala mazima ya Vikombe na medali kwa ajili ya washindi wa michezo mbalimbali ikiwemo mashindano ya kupiga menu yaani tonge nyama...


Siku hii ya wanafamilia wa Zain pia ilikuwa kilele cha Zain Staff Premier League...Pichani refa wa mchezo Othman Kazi akitoa maelekezo kwa wasakata kabumbu kabla ya mtanange kuanza...



No comments: