JOSEPH PAYNE AMECHAKACHULIWA??

Joseph Payne pichani alionyesha uvumilivu na ukomavu wa hali ya juu siku ya fainali ya Bongo Star Search baada ya kile kilichodhihirika wazi kuwa ubaguzi wa rangi.Payne ambaye alijizolea umaarufu katika shindano hilo kwa kuimba kiufasaha nyimbo za kiswahili alikumbwa na hali hiyo mara baada ya majaji wakiongozwa na Rita Paulsen kumshambulia yeye pamoja na mashabiki kwa kumpigia kura hali wakidai wanaacha kupigia kura vipaji vya ukweli.

Payne aliyekuwa na namba ya ushiriki BSS 07 alikonga nyoyo ya wapenzi wake bila kujali kashfa zote hizo na hadi usiku wa manane bado alikuwa akiongoza kwa kura upande wa Mtandao akiwa na asilimia 38.7 akifuatiwa na Mariam Mohamed(aliyetangazwa mshindi) aliyekuwa na asilimia 36.5."Watanzania acheni ushamba kumuona mzungu anaimba kiswahili"alisikika akisema Master Jay Producer mkongwe nchini ambaye kwa hadhi yake alitegemewa ajiheshimu na kutoa muongozo kama Judge ambaye ni mkufunzi wa muziki.Kwa kutoa 'judgement' ya kitaalamu huenda angetusaidia sisi 'washamba' kuona mapungufu ya Payne badala ya kumkashifu na kututukana.Kwa upande wake nae Rita alibaki kusema tu 'munaacha kupigia kura watu wenye vipaji mnapapatikia mzungu,kuna watu wanzihitaji milioni 30 kuliko hata yeye' hayo yalimponyoka pale Waziri Salum alipotolewa kuingia raundi ya pili.

Ninachojiuliza je,hawakuona kuwa Payne ni mzungu toka mwanzo??Je,kuonyesha ubaguzi wa wazi mbele ya watanzania kunamfanya Rita astahili huo u-madam aliojipachika?Je,hawajui kwa ushamba wetu tuliounyesha kumpigia kura Payne kwamba tungeweza kuuendeleza kwa kununua kazi zake??Je,kulewa pombe kazini ni halali??kwa kuwa majaji wawili(Rita na Master Jay) kati ya wanne walokuwa pale walikuwa wamelewa dhahiri.

Nawasilisha

No comments: