MACHO YOTE FAINALI ZA BSS LEO

Bongo Star Search Live majukwaani haikubaki nyuma
Bella Kombo ataondoka na milioni 30 leo??

Joseph Payne umahiri wake kuimba kibongo utampa uStar wa Bongo leo?

SHINDANO LA KUMSAKA KINARA WA MUZIKI LA BONGO STAR SEARCH leo linafikia ukingoni ikiwa ni baada ya miezi takriban miwili ya mchuano mkali wa vipaji.Wakiwa wamebaki washiriki watano ambao ni Joseph Payne(Mzungu),Bella Kombo,Waziri salum,Mariam Mohamed na James Martin usiku wa leo tutampata mshindi pale Mlimani City Hall.Fainali hii ya kukata na shoka itamtawadha rasmi Super Star wa Bongo kwa 2010 na kumwezesha kuondoka na kitita cha Milioni 30 taslimu na mazagazaga mengine kibao.....Usikose uhondo
huu !


No comments: