MLIMANI KWALIPUKA

Barrier ya polisi kuzuia njia ya kuingia SURVEY kutokea kiplefti cha Samnujoma Mlimani city..Asubuhi palikuwa hapatoshi
Ili kuingia Mlimani city kwa geti la upande wa survey imetubidi tuzunguke na kupanda juu ya msingi ulowekwa usawa wa Zebra kwa ajili ya waenda kwa ngoko.
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Leo kimenuka katika chuo kikuu cha Dar es Salaam,Mlimani mara baada ya polisi kulazimika kuzima maandamano ya siyo na kibali ya wasomi hao.Wanazuoni hao walikuwa na mpango wa kwenda kumuona Rais kumprizentia ishu zao mbali mbali ikiwemo ile maarufu ya ongezeko la mshiko yaani boom.
Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia walilazimika kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji hao na kisha kuzuia barabara mbili kuu za kuingilia na kutokea chuoni hapo baada ya tetesi kuwa Wasomi hao walopandisha mzuka wa kumwona Amiri Jeshi Mkuu wameamua kubadili route na kutaka kupitia gate la Ubungo chuo cha Maji Rwegarulila.


No comments: