KRUZ PARTY

FREE COCKTAIL TO THE FIRST 200 PEOPLE....DON'T THINK OF MISSING THIS...



MOROGORO ROAD KUNA MKONO WA MTU



Barabara yetu hii ya Morogoro kwa kweli inatumaliza..Hapa ni Kibaha kwa Mfipa kitu kimejibu fuso hilo a.k.a John Cena limefanya uharibifu na kumsaidia Israel Roho mbili on ze spot



BREAKING NYUUZ:MOTO SOKO LA MWANJELWA

Live kutoka Mbeya ni kwamba tunavyozungumza saa soko la SIDO Mwanjelwa Mbeya linateketea kwa moto na hakuna juhudi zinazoendelea za kuzima moto huo..

AJIRA KWA WATOTO

Kamera yetu ilimnasa mtoto huyu leo mchana maeneo ya Tabata akiwa kazini.Alipoulizwa na Nipenikupe alisema amepewa tenda ya kuhamisha kifusi hicho na anajipanga aanze kazi bila kulaza damu

DARAJA LA MTO KAGERA







Hili ni Daraja jipya la Mto Kagera...Kinachoonekana kama ngazi ni Daraja la Zamani la Mto Kagera lililovunjwa na Amin wakati wa vita....



KUMBUKUMBU YA VITA YA KAGERA

Pichani ni chasis ya lori ISUZU iliyopigwa bomu na majeshi ya nduli Idd Amin tarehe 3 February 1979 wakati tukiwa tunapeleka vikosi vyetu kumtandika Idd Amin Dada...Ukipita Mji wa Bukoba si vibaya kutembelea kumbukumbu hii murua ya historia yetu inayoonyesha jinsi ambavyo wazee wetu walijitoa kulinda na kutetea hadi ya Taifa



MNARA WA MASHUJAA WA VITA YA KAGERA

Nikiwa safarini Mtukula(Mpaka wa Bongo na Uganda) nilisimama kutoa heshima kwa mashujaa wetu wa vita vya Kagera..hapa nipo nje ya Mnara wa Kumbukumbu ya mashujaa



WABONGO TUPO HAPO??

Mabingwa wa kuegesha gari palipoandikwa 'usiegeshe gari hapa' na mabingwa wa kukojoa palipoandikwa 'usikojoe hapa' tungeyaweza haya

LADIES FIRST...KUBADILI TAIRI







Katika ule utamaduni wetu wa Ladies First basi tunaomba bidada ashuke kwenda kubadili tairi mbele ya Munyama huyo...


VITA DHIDI YA VVU

Katika mpambano na Ugonjwa wa Ukimwi ofisi hii imeamua kutumia majina ya condom kuelekezea watu msalani..Very creative kwa sana because kama wewe hutumii hizi vitu tutakujua tu utakavyoweweseka na kuingia Lady Pepeta wakati we ni dume...

Hii sasa iwe nchi nzima.

JOY@WORK

Habari njema hizi mngezipokeaje wadau...!!kitu cha Pombe dispenser kitakapo-replace Water dispenser...



HONGERA BARUANI MSHARE



PhD student Baruani Mshare received the prestigious International Dissertation Research Fellowship(IDRF) from the Social Science Research Council(SSRC).The fellowship will support his forest-related dissertation work in Tanzania.

Mtanzania mwenzetu Baruani Mshare anaefanya shahada yake ya Udaktari wa Falsafa katika chuo kikuu cha MICHIGAN Marekani amekuwa mmoja kati ya wanazuoni 77 duniani kushinda baada ya takriban watu 1200 toka vyuo 128 ku-apply..kwa habari zaidi bofya hapa

www.snre.umich.edu/highlights/2011-04-12/phd_student_baruani_mshale_receives

ENZI ZA MAPAMBANO

Nimekuta Picha hii ya kipindi cha kampeni katika ukuta wa Facebook kwa mpambanaji Killian.Leo Mnyika ameshusha hotuba nzito ya bajeti mbadala wizara ya Nishati na Madini akiwa waziri kivuli...soma hotuba nzima katika www.mnyika.blogspot.com


VIFARANGA KWA BEI POOOAAA..

Kwa wajasiriamali wafugaji hizi ni habari njema sana kwenu...Wahi sasa kabla hujachelewa.

MAANDAMANO??







Unadhani tupo katika maandamano??La hasha....hapa tupo Ubungo Bus Terminal ya Ndege jijini Mwanza a.k.a Uwanja wa Ndege wa Mwanza...Unapotangaziwa kwa bashasha kupitia kipaza sauti kuwa sasa Ndege yako iko tayari kuondoka maana yake ni kwamba jiandae kuchanganya ngoko na kukatiza uwanja kwa ngondi hadi kuleeee unapoziona Ndege...Hii ni staili mpya ambayo naambiwa imedumu kwa muda sasa..Hao jamaa wenye vi-refletor ndo wanaotuongoza njia katika kamsafara haka.....!!!


TIT=This is Tanzania